TAWLA YAONGEZA JITIHADA ZA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI NCHINI




Chama cha wansheria wanawake nchini Tanzania TAWLA, kimeanzisha utaratibu wa msaada wa namna jamii inavyoweza kupata huduma za kisheria kwa kuanzisha utaratibu wa wanasheria wasaidizi.








Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Aisha Bade amesema wanasheria wasaidizi watakuwa wanaelekeza jamii namna ya kupata huduma za kisheria hasa kwa makundi yenye uhitaji wakiwemo wanawake, watoto, wajane, waathirika wa ubakaji pamoja na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.


Kwa mujibu wa Bi. Bade, mpaka sasa TAWLA imeshafundisha na kuandaa wanasheria wasaidizi 412 waliosambazwa maeneo mbali mbali nchini, ambao uwepo wao utapunguza garama ya kupta huduma za kisheria pamoja na pengo la uhaba wa huduma hiyo katika jamii.



Mara nyingi watu wananyimwa haki au wanakosa hki kwa kukosa misaada wa kisheria kutokana na upatikanaji wake ni gali na iko mbali na jamii hivyo hawa wasaidizi wa kisheria watatusaidia kuwafikia jamii kwa haraka zaidi n a bila garama yoyote” amesema

Pamoja na kuazishwa kwa huduma hiyo bado vongozi wa serikali hasa kwenye ngazi za mikoa hawatoa ushirikiano wakutosha kwa wasaidizi wa kisheria hali inayo rudisha nyuma jitihada za masuala ya kisheria, hivyo wananchi na viongozi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano ili tuwe na taifa lenye haki na usawa.



EmoticonEmoticon