Tuesday, March 24, 2015

JIHADHARI NA MATAPELI AJIRA ZA WALIMU WAPYA 2016, SOMA HAPA

                           
                                             


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA
SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
MWAKA 2015/16.
 JIHADHARI NA MATAPELI

Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.

Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.

Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.


Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
23 Machi, 2015


Wednesday, February 25, 2015

TCRA YATOA MAAGIZO KWA MAKAMPUNI YA SIMU JUU YA TOZO ZA VIFURUSHI VYA MAZUNGUMZO, MESEJI NA INTANETI


KUHUSU TOZO KWENYE SEKTA YA TEHAMA

Katika wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo ambayo yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku zijazo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, miongoni mwa kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta inazozisimamia kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na viwango vya huduma, bei ya huduma na kuhimiza ushindani na ufanisi wa kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake, TCRA inawajibika kupitia na kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta na kuchukua hatua dhidi ya chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au hasi.

Monday, August 18, 2014

MAUAJI YA ALBINO YAIBUKA KWA KISHINDO. DKT MENGI ATOA MILIONI 10 WAUWAJI WAKAMATWE: SERIKALI NAYO ICHUKUE HATUA KUKOMESHA MAUAJI HAYO.

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/7e5cebf75b882ff6cf47e51c7f3ca25d_XL.jpg 
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kuwa atashirikiana na jeshi la Polisi nchini Tanzania Kutoa zawadi ya shillingi millioni kumi kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu waliyomkata mkono Munghu Mugasa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi katika kijiji cha Buhekela Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora pamoja na kumuua mume wa mama huyo nakujeruhi watoto wao wawili.

Dkt. Mengi ameyaeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari na kueleza kuwa IPP itachukua jukumu la kuwasomesha watoto wawili wa familia hiyo ambao baba yao ameuwawa na mama yao kuachwa na ulemavu huku akilitaka jeshi la Polisi nchini kuhakikisha kuwa wanawatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hilo. 
“Unge jiskiaje endapo aliye uwawa angekuwa ndugu yako ama aliye katwa mkono ni ndugu yako? Inasikitisha sana. Mimi sina la kufanya ila naomba sana serikali na hasa jeshi la polisi Mkoa wa Tabora kufanya msako kuwakamata waliohusika na tukio hili lakusikitisha” Amesema Dkt Mengi.

Friday, August 15, 2014

"UNYWAJI WA POMBE NA UVUTAJI WA SIGARA KILA SIKU HULETA KISUKARI"

http://www.prevention.com/sites/default/files/EatToBeatDiabetesGoGuide-620px.jpg
Wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania imebaini asilimia 13.7 ya wananchi wanadalili ya ugonjwa wa kisukari kwa Tanzania bara hali inayosababishwa na uvutaji wa sigara au tumbaku na unywa wa pombe kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi na lishe duni.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa asilimia 14.5 wanakunywa pombe kila sikuhuku asilimia 36 wanavuta sigara. Kuhusu masuala ya uzito kupita kiasi ni asilimia 24 wanauzito usio hitajika huku asilimia 30 wameonekana kuwa na ongezeko la msukumo wa damu.

Akizungumza wakati akizindua utoaji wa huduma za bure zinazotolewa na Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya jeshi hilo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam kwa muda wa siku 3, Kaimu mkurugenzi wa tiba wa wizara hiyo Dr.Ayoub Magimbu amewataka wananchi kuipunguza matumizi ya vitu ambavyo vitahatarisha maisha yao.

Thursday, July 3, 2014

JWTZ YAWA MIONGONI MWA VIKOSI BORA 35 VYA MAJESHI DUNIANI


Majeshi Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri.
 
Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake miongoni mwa majeshi bora duniani.

Chini ya kichwa cha habari “35 Most Badass Elite Fighting Units from Around the World” mwandishi, Micky Wren anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani, yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi na yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo mkubwa.

Wednesday, February 19, 2014

BUNJU SISTERS GROUP INAKARIBISHA WANACHAMA WAPYA


Kikundi cha Bunju Sisters Group kimekuwa kikikutana kila mwisho wa mwezi kwaajili ya kupea taarifa mbalimbali za chama, mapato na matumizi pamoja na mipango ya baadae ya kikundi chetu

Kuanzia kushoto ni Wendy muweka hazina , wapili ni Suzan Nzota Katibu na wamwisho ni Loyce Joseph mwenyekiti wa kikundi
Japo tumekuwa na misukosuko mbalimbali ikiwemo ya misiba ya wanafamili wa wanachama wetu, wengine kutengana na kikundi kuelekea vyuoni kwa masomo pamoja na ubize wa kazi za kila siku lakini Umoja na urafiki bado unadumu kati yetu

Kutoka kushoto ni Bibiana, Suzy na Janeth Jackson

Pole kwa Janeth Jackson aliye mpoteza Mume wake Kipenzi, Pole kwa Rosemery aliye fiwa na baba yake kipenzi kwa upande mwingine Hongera kwa Bibiana aliye mwozesha mdogo wake na Lucy aliye baatika kupata mtoto wa kiume mungu awape maisha marefu sana wana kikundiMara nyingi tumekuwa kwenye vikao vya usiku, kutoka out kubadilishana mawazo na mara zingine tunatembeleana ili kuzidisha mshikamano wetu. Tume weza kukopeshana na kusaidia kwenye matatizo mbalimbali kama msiba na harusi na kiuchumi.

Kutoka kushito ni Janeth, Loyce Joseph, Bibiana na Lucy
Mwenyekiti wa Bunju Sisters Group anapenda kuwkaribisha kina dada wote wenye nia ya maendeleo na kusaidana, kupata marafiki katika eneo la Bunju kuwasilina nasi kupitia Simu no. 0659 269416 kwani huu ni muda wa kukaribisha wanachama wapya. Vigezo na masharti nivya kawaida Karibu.

Tuesday, February 11, 2014

MAFUNZO KWA WALIMU WALIOPO KAZINI MKOANI MWANZA YAFUNGULIWA RASMI NA KATIBU MKUU ELIMU


Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi Prof. Sifuni Mchome amefungua rasmi mafunzo kwaajili ya walimu walioko kazini katika mkoa wa mwanza ambapo ameweza kutembelea baadhi ta vyuo na shule mkoani hapo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyakurunduma iliyoko jijini Mwanza ambapo alitembelea shule hiyo kuona ujenzi wa miundombinu (maabara, vyooo, ukarabati wa madarasa na tanki la maji)