LOVE & RELATIONSHIP

 NI MUHIMU KUZINGATIA WAKATI WA TENDO LA NDOA

Mara nyingi watu hufanya mapenzi kwa jinsi ambavyo anajua yeye, pengine kwa kuona kwenye picha za ngono au kwa kufundishwa na mwenza wake au pia niujuzi tu wa mtu mwenyewe akajikuta ni mtaalamu sana au anauwezo mkubwa wa kumfurahisha mwenzawake.

Kutokana na mazoea kila mtu anaweza kusema anayajua mapenzi au anaweza mapenzi, lakini watu Wengi huchoka sana mara baada ya kufanya mapenzi pengine ametumia nguvu nyingi au anakosea mambo fulani anapokutana na mwenza wake, lakini kuna aina mbalimbali ambazo unaweza kufanya mapenzi bila kuchoka wala kulalamika maumivu.

Hii itawahusu sana wanawake kwani ndio wanatakiwa kutoa ushirikiano mkubwa sana katika tendo hili, mbwembwe za mwanaume aziana maana mpaka pale mwanamke aonyeshe ushirikiano na ushirikiano huu ndio ukamilisha tendo lenyewe kinyume na hapo niubakaji.

Kuna kina dada wengi wana lalamika juu ya mapokeo ya wanaume wao wanapokuwa kwenye mambo kwani wanaume wengine wanajali hisia zao tu kiasi kwamba mwanamke anakuwa msindikizaji tu kila mara. muda mwingine mwanamke huchoka sana hata mchezo mmoja tuu kutokana na maandalizi na utendaji usio vutia hisia zake

Wanaume wengi wanajali mwanzo wa mchezo kwamba atakuandaa, lakini asiangaliye je bado hisia zako ziko vile vile au umeshapoteza ladha katikati ya mchezo aongeze ujuzi, kwani kuna wakati mwanaume aweza kuwahi na akaendelea ili muwe sawa lakini umeongeza ujuzi au mwendo ni ule ule? hili ni lakuzingatia sana japo wengi wanajisahau. Si mwanzo wa mchezo ndio manjonjo yaishie hapo kila hatua inautofauti wake hivyo kumfanya mwenza wako kufurahi zaidi na kukupa raha unayoihitaji kikamilifu

Endapo mwanamke atawai kumaliza kabla ya mwanaume pia yahitajika mbwembe kumuweka karibu zaidi na mwendelezo wenu ila kama utaburuza tuu haina maana kwani mwenzako tayari alisha maliza zamani na hana hamu tena hapo ndipo kuchoka na kufanya kwakujilazimisha kunaanza, hivyo unapaswa kuwa mtundu kwa kila hatua unayoendanayo 

Mwanaume mahiri kila anapobadili style ni lazima atumia hata dakika 5 kumuandaa tena mamaa, ili kila anachofanya kiende sawa 
sawa hivyo kuongeza raha zaidi na kuepusha kuchoka wala kupata maumivu kabla na baada ya tendo. kwanini uumie katika uwanja wa raha, zingatia kila hitaji ni muhimu. hapa kuna video ikielezea mambo ambayo mwanamke au mwanaume atakiwi kufanya anapokuwa kwenye tendo la ndoa. hii inawahusu wanawake na sio wasichana.


VIDEO HII INAELEKEZA WANAWAKE KWA WANAUME MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA    TENDO LA NDOA NA HUU NIKAMA MFANO TU ILIOTUMIKA

*******************************************

        UPWEKE SIO KIGEZO CHA KUTOFURAHIA VALENTINE DAY

 

Msomaji wa safu hii, naamini mambo yanaenda kama ulivyo panga nakama sivyo basi usilaumu ndivyo ilitakiwa iwe. Valentine day nimiongoni mwa siku maarufu sana Duani nakutakia Furaha na Amani ndani yamoyo wako, tena niko pamoja na wewe katika kuhakikisha siku yako inamalizika kwa Fuhara tele

Siyo wote ambao wanaijali sana siku hii lakini kunawengine huijali sana, kama wewe nimiongoni mwa kundi lolote katiya hayo hii inakuhusu kwa namna moja amma nyingine. Kusherekea siku ya wapendanao hali ukiwa mpweke lakini bila kuhisi tofauti katiyako na wale waliombeleyako yaani wapendanao

Nihali mbaya hasa kwa wale ambao siku kama hii wakati uliopita walikuwa kwenye furaha na wapendwa wao maranyingi siku kama hii hurudisha kumbukumbu nyingi zahuzuni na kuumiza, lakini kumbuka haupo pekeyako nasio wewe tu unaye pitia hali hiyo.

Kuna wale ambao wako nawapenzi wao siku hii lakini hawafurahii kabisa kuwa nao, pengine chaguo lake alishatoweka na aliye naye nikwasababu huwezi kuyakimbia mapenzi daima,



Kundi lawatu kama hawa nao hawafurahii siku hiyo au hawapendi kujishugulisha nayo.

Kikubwa ilikuponya moyo wako, unatakiwa kujua kuwa Siku ya tarehe 14 Feb (Valentines Day) siyo sikupekee inayoweza kukufanya uyajali mapenzi au siyo siku pekee yawapendanao, unaweza kufurahi na kuuponya moya wako kwa furaha katika siku yoyote ile ambayo wewe nimuhimu kwako

Mara nyingi kama unahisi utapatwa na upweke, nimuhimu kuwa na njia yakuifanya iwe tofauti kwako kwa kuwa kribu na familia au kupanga safari ya watu kadhaa ambao kati yenu sio wapenzi ilikufanya hisia zenu kuwa kitukimoja kiasi kwamba mmoja wenu asihisi upweke moyoni.

Kuifanya siku hii kuwa tofauti na siku iliyopita mabyo inakupa kumbukumbu mbaya, ni wewe mwenyewe kujenga mazingira tofauti nayale yalio pita, kaa karibu nafamiliya yako, andaa japo zawadi ndogo kwaajili yao hii itakupa picha nyingine ya siku hii na kufuta kumbukumbu za nyuma.


Lakini sivizuri wewe kwende kwenye ukumbi au mahali ambapo uliwahi kwende na X- wako hasa katika siku hiyo kwani itarejesha kumbukumbu na majonzi moyoni nakujikuta ukienzi huzuni kwani mahali pale panaweza kukuondolea furaha.

Wengi hupenda kuwa wish X-Lover katika siku hii, kama unajua moyo wako simwepesi kuhimili nibora usifanye hivyo tafuta njia mpya ya kuupa furaha moyowako. Mapenzi nikama mvua ikinyesha hutawala eneo lote sio kama maji yabomba, nimuhimu kujipa ujasiri na kuufundisha moyo wako kutulia nakukubali halihalisi, pia ujue kuachana au kuvunjika kwa mapenzi sio mwisho wa upendo.

Badilisha mtazamo wako juu ya siku hii, Epuka kuifanya siku hii kama siku muhimu sana kwako, kama unaratiba zingine basi endelea nazo kama kawaida iliusiweze kujiisi uliye mpweke. Tambua unapokuwa mpweke kwa kipindi Fulani aimaanishi upendo umekukimbia au wewe hustahili.

Upweke wako uondoe kwa kujiandalia mazingira ya furaha, waweza kwenda mahali unapo papenda ilitu kuifanya akiliyako kuwa bize na mambo mengine. Muhimu kumbuka hauko pekeyako wapo watu wengi waliokuzunguka ambao wanakupenda na kukujali japo kwa moacho sirahisi kuwahona 


Ujasiri ndio njia nzuri yakupoteza upweke, sivyema kuitafuta furaha kwanjia ambazo zitaleta madhara kwako,nakuzidi kukufanya kuyachukia mapenzi





Nakusihi tuliza akiliyako naujaribu kufikiria njia ya kukupeleka katika hatua nyingine zaidi ambayo itakupa furaha mudawote. Kwa hitimisho tu nikwama furaha hukamilishwa na wewe mwenye muhimu kuzingatia mengi niliyo kupatia

 Posted on: February 2013

 ********************************************

NANI MWENYE HAKI YA KUSHIKA SIMU YA MPENZI WAKE?? KATI YA HAWA WAWILI??

Kundi la kwanza ni ~ Wanandoa ambao tayari ni mume na mke au wanaishi pamoja kama wanafamilia.

Kundi la Pili ni ~ Walio kwenye Uchumba ambao hawaishi pamoja au hawaja oana lakini wanatarajia kuingia katika ndoa.

                  Swali langu katiya makundi hayo mawili ni kundi lipi linauhalali wa kuwa huru na simu ya mkononi ya mpenzi wake, bila kujali kama ni mwana mke au mwanaume.

Swala la simu miongoni mwa wapenzi huwa lina utata na matatizo mengi, Campasvision imefanya utafiti katiya makundi hayo mawili kwa kuuliza maswali baada ya kubaini kuwa kuna kundi moja linaamini lina uhalali wa kuwa huru na simu ya mpenzi wake, huku kundi lingine likidai akuna uhalali wakuwa huru na simu ya mpenzi wako kwa sababu tofauti tofauti ambazo walizitaja 

Tukianza na kundi la kwanza ambalo kila mtu anamtegemea mwenzake, yani mume na mke kwani nikama familia au umoja wenye mambo mengi yanayo fanyika kwa pamoja na kuwa jumuisha pamoja, tusema nifamilia pengine yaweza kuwa na watoto au lah.

Wengi wa watu niliofanya nao mahojiano katika kundi hili ambao wote walikuwa walio oa na kuolewa, kundi hili walisisitiza juu ya kuwa huru na simu ya mwenza wako kwa sababu nyingi na zilizo kuwa na msingi kabisaa, 

Hakuna aliye kuwa na sababu ya kwa nini mke wake au mume wake asishike simu yake, aidha kwa idhini au bila idhini kutokana na kuwa tayari wao nifamilia moja mipaka kama hiyo aijengi familia. Na endapo kutakuwa na mtu anamkatazia mke au mume wake kushika simu yake ya mkononi basi siyo mwaminifu katika mapenzi yake na kwakuwa simu ndio mficha siri zetu basi wengi wanahofia kuumbuka, ilikuji ficha basi anaamua kuwa mkali kwenye simu yake.

Kundi la Pili ni la wale wachumba ambao wanatarajia kuingia katika ndoa, ila bado kila mtu anakaa peke yake au anakaa na wazazi wake. majibu niliyo pata toka kwenye kundi hili kwa wasichana na wavulana halikuwa la moja kwa moja, kwamba ninani mwenye uhalali wa kushika simu ya mwenza wake kati ya kundi la kwanza au kundi la pili

Wengi wa kundi hili waliwajibia waliokwenye ndoa kuwa ndio wanastahili kushika simu ya mwenziwake. Lakini miongoni mwao hawakuwa tayari kusema kama wanaona uhalali wa kushika simu za wapenzi wao, na hawa walikuwa wasichana kwa wavulana ambao bado wako kwenye uchumba

Nilicho kibaini ambao ni utofauti wa makundi haya mawili nikwamba, Kundi la kwanza tayari limeshajiwekea malengo na uhakika wa mahusiano yao lakini kundi la Pili bado hawana msimamo na malengo kwenye mahusiaono yao ndio maana wakashindwa kutoa jibu la moja kwa moja, na swala la kushika simu za wapenzi wao au mpenzi kushika simu yake ilikuwa kasumba kubwa naamini bado hawajawa waaminifu na msimamo wa mahusiano yao

Kitu cha msingi ambacho kila mtu anatakiwa kujua anapokuwa katika mahusiano, nijukumu la kulinda penzi na kuwajibika kwa mwenza wake bila kujali wewe ni mume/mke au wewe ni mchumba tu, kwani hakuna anaye ingia katika maisha ya ndoa bila kuanzia katika uchumba.

Kwa mtu ambaye ni mwaminifu hakuna sababu ya wewe kuficha simu au kuzima simu hata kuweka password na vikwazo vingine ambavyo vinapelekea kuweka mipaka kati ya wapenzi wetu, kumbuka kwamba kuwa muwazi katika mambo yako hujenga mahusianao na kuleta uaminifu kati yenu.

kulingana na mada yetu hakuna asiye kuwa na uhalali wakushika simu ya mwenzi wake kama tayari umeamua kuwa huyu ni wangu wa maisha, hasa kwa wale walioko kwenye ndoa. si vyema kumkataza mwenza wako kushika simu yako na kama hili nitatizo ambalo unahisi linakukera sana pale mpenzi wako anaposhika simu yako au pale anapokukataza kushika simu yake. kila kitu kina sababu na maana yake ni bora kuzungumza ilikuweka mambo sawa 

Kikubwa cha kufanya nikupunguza mabavu na maamuzi ambayo yanaegemea upande wako bila kujali mwenzako anajisikiaje au atanielewaje katika hili swala... kuwajibika katika kulinda mahusiano kwa kila namna ni jukumu la kila mmoja wenu. Tuwe watu wakuweka vitu wazi na kusisitiza uhaminifu miongoni mwenu

Posted on: January 2013

******************************************

JE MUONEKANO WA KITANDA    HUONGEZA HISIA NA HAMU YA  MAPENZI?????

Miongoni mwa vitu ambavyo binafsi na vipa heshima ni Mapenzi,japo tunatofautiana sana kimtazamo na imani ya mtu mmoja mmoja juu ya swala zima la mapenzi.ila lisilo pingika miongoni mwetu nikuwa Mapenzi yanatawala kila mahali.

Kuna watu huamini msichana mzuri au mwanaume mwenye muonekano wakuvutia huongeza hisia za mapenzi hasa wawapo kenye mahaba, kwamba hisia zake zinajengwa na muonekano wa msichana au mwanaume aliye naye, kwa wengine hiyo sio hoja ..zaidi uamini mapishi ya mtu mwenyewe awapo kitandani ndio hujenga hisia zake na kumfanya ajisikie raha zaidi.lakini pia kuna wengine ambao haya yote kwao yana kipaumbele na huyazingatia.

Lakini mimi sito egemea upande wa mvuto na uwajibikaji tuwapo kwenye mahaba. Swali la msingi ni kwamba JE MUONEKANO WA KITANDA HUONGEZA HISIA ZA MAPENZI?, jibu ni ndio,endapo kitanda kitakuwa kisafi na chumba kikawa na muonekano mzuri ni dhahiri kuwa mtu lazima hisia zako zitakusukuma kwenye mahaba kutokana na hali ya usafi iliyo tawala au kulala usingizi mnono

Hisia ya mwanadamu inaongoza na Akili nasio Mwili, kama utajenga hisia zako kutoka mwilini bas nidhahiri kuwa wakati mwingi waweza usifurahie tendo la ndoa au mapenzi. katika utafiti nilioufanya mimi ulinipa jibu kuwa ambao hawatosheki kimapenzi niwale wanao ziachia akilizao kutaka kufanya mapenzi bila kuangalia uwezo, nafsi ,hisia na afya yao ya kukutana kimwili, kwani ndani ya hivyo vitu ambavyo atuvizingatii ndio hujenga mazingira salama katika mapenzi. uwezo wakwanza ni mahala ambapo unakutana na mwenzi wako ndipo mengine kama hisia hufuata.

Daima jifunze kuiandaa akili katika hali ambayo ungependa, wataalamu wa rangi nao wakalonga kuwa kuna rangi ambazo uongeza nakshi katika mapenzi. Muimu kuzingatia hali ya kitanda chako..Kama mumeo akitoka kazini na amechoka sana basi mwanamke una mbinu nyingi sana za kumfanya aamke na kukusogelea bila hata wewe kumhamisha, kwanitayari umemjengea uwezo nabaadae nafsi yake husukuma hisia zake.

Muonekano wa kitanda chako nilazima kiwe kwenye hali ya usafi, kuanzia mashuka yako, mpangilio wa chumba chenyewe na usafi wa ujumla wa chumba chako. Muimu kuzingatia Rangi ambazo mashuka yako yanatakiwa kuwa nayo..Wataalamu wanasema Rangi ya Zambarawe (Purple, Blue), maranyingi rangi zinazotuzunguka huwa na maana sana, katika swala la usafi aliitaji mwenye uwezo na asiye na uwezo.

Kitanda kichafu huongeza uchovu kama babaa atalala asipo hamka usilalamike...zingatia hali ya chumba chako hawezi kulala mpaka akusalimie, tena mkimaliza mahaba uchovu hutoweka kutokana na usafu wa chumba na hewa nzuri.Nitalisisitiza sana kwa wanawake au wadada ambao mara nyingi ndio waandaaji wa mahali pakulala,ila aimanishi wanaume hawausiki katika hili. kwakuzingatia hayo utakubali kuwa Kitanda huongeza hamu ya mapenzi.


EmoticonEmoticon