TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR (ZEC) IMEFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar salim jecha salim ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa madai kuwa kumekuwepo kwa kura nyingi kuliko idadi iliyopo kwenye daftari la wapiga kura.
Akitangaza suala hilo mwenyekiti wa zec amesema kumetokea kuwepo kwa dosari nyingi kwenye upigaji kura jambo ambalo amelitaja kuwa sio wa haki.
"Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika." amesema salim jecha
Amesema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukuwa vitambulisho vyao vya kupigia kura".

Wakati huo huo, mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha chadema na ukawa edward lowassa amesema hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na tume ya uchaguzi nchini tanzania nec.

Lowasa ametoa madai kuwa kuna udanganyifu uliofanyika nakuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura, pia lowassa ameongezea kuwa maeneo yote ambayo walipata ushindi matokeo yamechelewa kutajwa. 


EmoticonEmoticon