BUNGE LAVURUGIKA NA KUAHIRISHWA , KAULI YA WAZIRI MKUU MHE. PINDA YASUBIRIWA KWA HAMU



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo asubuhi amelazimika kusitisha shughuli za bunge baada ya wabunge kutaka serikali kuahirisha mchakato wa kura ya maoni pamoja na kutoa taarifa ya uandikishwaji wa wapigakura kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa BVR.




Wakichangia hoja bungeni Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman Jaffo na Mbunge wa Ubungo Mh. John mnyika wametaka suala hilo lijadiliwe kama dharura na kutolewa majibu na serikali kuhusu hatama ya mchakato huo.

Taharuki ilizuka baada ya Spika wa Bunge hilo Mhe. Makinda kutaka kuzitupilia mbali hoja hizo. Wabunge walianza kupiga kelele kutaka majibu ya serikali papo hapo na ndipo Spika wa bunge alilazimika kuhairisha kikao hicho mpaka jioni ambapo leo ni kikao cha mwisho cha bunge hilo.

Mnyika “ Nimesimama kupata Idhini kwa mujibu wa kanuni kuomba shuguli za mbunge zisitishwe na badala yake tujadili zoezi la uandikishwaji kwani mpaka sasa zoezi halijakamalika hata kwa mkoa mmoja, hivyo Waziri mkuu kwakuwa yupo hapa Bungeni atupe majibu nini kinaendelea” Amesema Mnyika

Spika “Hoja hii na ile ya kwanza zinafanana, majibu mtajibiwa baadae katika kikao cha jioni” Alisema spika. Aidha wabunge wa Upinzani walionesha nia ya kutaka kujua hivyo kupiga kelele kwakusema “Tuna taka Majibu” hali iliyopelekea spika wa bunge kuahirisha Bunge hadi jioni.


Bunge la jioni tunatarajia Mhe. Mizengo Pinda Waziri mkuu wa Tanzania kutoa tamko la serikali nini hatma ya mchakato wa kupigia kura katiba inayopendekezwa.
Kura ya maoni inategemewa kupigwa tarehe 30 mwei wa 4, 2015 mwaka huu licha ya kutokuwepo kwa uboreshaji wa daftari la kupiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa BVR.



EmoticonEmoticon