"UNYWAJI WA POMBE NA UVUTAJI WA SIGARA KILA SIKU HULETA KISUKARI"

http://www.prevention.com/sites/default/files/EatToBeatDiabetesGoGuide-620px.jpg
Wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania imebaini asilimia 13.7 ya wananchi wanadalili ya ugonjwa wa kisukari kwa Tanzania bara hali inayosababishwa na uvutaji wa sigara au tumbaku na unywa wa pombe kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi na lishe duni.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa asilimia 14.5 wanakunywa pombe kila sikuhuku asilimia 36 wanavuta sigara. Kuhusu masuala ya uzito kupita kiasi ni asilimia 24 wanauzito usio hitajika huku asilimia 30 wameonekana kuwa na ongezeko la msukumo wa damu.

Akizungumza wakati akizindua utoaji wa huduma za bure zinazotolewa na Jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya jeshi hilo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam kwa muda wa siku 3, Kaimu mkurugenzi wa tiba wa wizara hiyo Dr.Ayoub Magimbu amewataka wananchi kuipunguza matumizi ya vitu ambavyo vitahatarisha maisha yao.
Kaimu mkurugenzi Dr.Magimbu aliyazungumza hayo akimwakilisha waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr. Seif Rashidi wakati wa uzinduzi huo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Naye Brigedia General Dennis Jenga ambaye ni mkuu wa tiba JWTZ amesema jeshi hilo linajivunia kwakuwa na madaktari zaidi ya 200 suala ambali linaiwezesha jeshi hilo kuhudumia watendaji wake na wananchi kwa ujula.

Brigedia General Jenga ameongeza kuwa kuanzia hii leo katika viwanja vya mnazi mmoja watatoa huduma za afya bure ikiwa ni maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya jeshi hilo. Nakuwataka wananchi kuhudhuria viwanjani hapo kwaajili ya kupata huduma bure.

Huduma zitakazo tolewa viwanjani hapo nibamoja na upimaji wa VVU;Uchangiaji damu wa hiari magonjwa ya kinywa na meno magonjwa ya mamcho pamoja na kufanya vipimo vya uzito na kujua kiwango cha damu mwilini.





EmoticonEmoticon