MAUAJI YA ALBINO YAIBUKA KWA KISHINDO. DKT MENGI ATOA MILIONI 10 WAUWAJI WAKAMATWE: SERIKALI NAYO ICHUKUE HATUA KUKOMESHA MAUAJI HAYO.

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/7e5cebf75b882ff6cf47e51c7f3ca25d_XL.jpg 
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kuwa atashirikiana na jeshi la Polisi nchini Tanzania Kutoa zawadi ya shillingi millioni kumi kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu waliyomkata mkono Munghu Mugasa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi katika kijiji cha Buhekela Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora pamoja na kumuua mume wa mama huyo nakujeruhi watoto wao wawili.

Dkt. Mengi ameyaeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari na kueleza kuwa IPP itachukua jukumu la kuwasomesha watoto wawili wa familia hiyo ambao baba yao ameuwawa na mama yao kuachwa na ulemavu huku akilitaka jeshi la Polisi nchini kuhakikisha kuwa wanawatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hilo. 
“Unge jiskiaje endapo aliye uwawa angekuwa ndugu yako ama aliye katwa mkono ni ndugu yako? Inasikitisha sana. Mimi sina la kufanya ila naomba sana serikali na hasa jeshi la polisi Mkoa wa Tabora kufanya msako kuwakamata waliohusika na tukio hili lakusikitisha” Amesema Dkt Mengi.

Endapo wahusika wakikamatwa nivyema waulizwe nikinanani wamewatuna ama waganga wanao jihusisha na vitendo hivi waulizwe waliwatuma kina nani na pindi wakiwataja hatua zichukuliwe isiishie kwa waliokata Albino mkono bali kwa waliohusika pia” Hii itatoa nia ya thati kwa serikali kupambana na mauaji haya yakusikitisha. Amesema Dkt Mengi

Wakati huo huo mashirika na taasisi mbalimbali za kutetea haki za binanamu ikiwa ni pamoja na Chama Cha Albino Tanzania (TAS), Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Taasisi ya under the same sun(UTSS),pamoja na mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wameitaka serikali kuchukua hatua za haraka sasa na wala sio kuishia kukemea huku mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yakiendelea .


Kwa muda wa siku 10 sasa katika maeneo mbalimbali nchini kumekuwa na ripoti za kuuwawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na imani za kishirikina huku wauwaji wakitokomea kusiko julikana na mauji na kukatwa viungo kwa walemavu wa ngozi vikiendelea kuripotiwa.


EmoticonEmoticon