MAKAMPUNI YANAYO CHUKU RUSHWA NA KUTOZA FEDHA NYINGI KINYUME NA KIWANGO HUSIKA WAKATI WA KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI KUSHUGULIKIWA


Wakala wa nishati vijijini REA, imeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma kuwa baadhi ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa wateja ili kuwaunganishia huduma hiyo.



Mkurugenzi mkuu wa REA Dkt. Lutengano Mwakahesya, amesema hayo katika mahojiano na East Africa TV, ambapo amewataka wananchi kutokubali kutoa rushwa kwa kampuni zinazounganisha huduma hiyo vijijini.

Kwa nini uchukue rushwa kwa mwananchi wa kijijini ambaye maisha yake ni bado yana mahitaji mengi, hili suala sio zuri kabisa na Waziri wetu (Mhe. Sospeter Muhongo) ameshatoa kauli kuwa nikinyume cha taratibu” amesema Lutengano

Aidha Dkt Lutengano ameongeza kuwa watumishi wa kampuni zilizobainika kujihusisha na rushwa, watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na tuhuma zao kufikishwa kwenye taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, jeshi la polisi na kwa mamlaka ya udhibiti wa manunuzi katika sekta ya umma—PPRA, huku


Hatahivyo Dkt. Lutengano amesema nihaki kisheria kwa mwananchi kulipwa fidia kabla ya miradi ya umeme kupita kwenye maeneo yaohivyo kuzidi kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali kupitisha umeme kwenye maeneo yao huku dhathmini ikifanyika ya kuwapa fidia wale ambao mazao yao yameharibiwa kwa kupisha miradi ya umeme.


EmoticonEmoticon